Mvua yafunika Barabara |
MVUA inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, imesababisha baadhi ya maeneo kujaa maji na kusababisha foleni na baadhi ya shughuli kusimama kwa muda mrefu.
Mvua hiyo iliyo anza majira ya saa saba mchana imeathiri shughuli nyingi za biashara hasa kwenye meneo ya Mbezi Beach Afrikana. Gari zimekwama barabarani kwa zaidi ya saa moja, hakuna gari inakwenda wala kurudi.
Maeneo mengine yaliyodaiwa kukumbwa na kadhia ya mvua hiyo ni Tegeta A kuanzia kwa Ndevu kuelekea Chuo Kikuu cha Mzumbe kuteremka Kunduchi Silver Sands.
Geri iliyofunikwa na mavi ya mvua patika eneo la Mbezi Afrikana |
Aidha maeneo mbalimbali ya jiji hilo yaliyokumbwa na mvua hiyo yameonekana kujaa maji.
0 Comments