Balozi Polepole akiwa na baadhi ya makamanda wa Jeshi la Tanzania na Malawi. |
Na Ephraim Mkali Banda-Blantyre
Balozi wa Tanzania nchini, Malawi Humphrey Polepole amesema
sehemu ya kwanza ya msaada wa kibinadamu kwa Malawi, umefika na tayari umekabidhiwa kwa wahusika.
Tayari Helikopta mbili za Kijeshi zilizobeba Madaktari ambao wanakwenda kuwa sehemu ya operesheni ya uokozi na vifaa vya kibinadamu wamewasili.
"Kwa niaba ya Wananchi wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, leo tunapeleka sehemu ya kwanza ya msaada wa kibinadamu kwa nchi ya Malawi, Helikopta mbili za Kijeshi na Madaktari ambao wanakwenda kuwa sehemu ya operesheni ya uokozi kufuatia madhila yalisababishwa na kimbunga Freddy katika Mkoa wa Kusini.
Polepole amenukuliwa akisema VIVA Mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na Malawi
Walioshiriki kupokea Masada huo wa kibinadamu ni Waziri wa Ulinzi wa Malawi Harry Mkandawire na Mkuu wa Jeshi la Malawi Vincent Nundwe na Balozi Polepole.
Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Malawi na Tanzania ni ya mda mrefu kutoka kipindi cha utawala wa Hayati Mwl. Julius Kambarege Nyenyere na Dkt. Heatings Kamuzu Banda.
Mahusiano hayo yamesababisha kuwapo kwa muingiliano mkubwa wa wananchi wa Malawi na Tanzania, na inaelezwa kuwa wananchi wengi wa Malawi wanaishi zaidi Dar es Salaam.
Aidha nchini Malawi watanzania wengi wanaishi kwenye eneo la Mzuzu ambako wamepewa soko la kufanyia biashara zao lijulikanalo kama "Taifa".
0 Comments