Rais wa Korea KaskaziniKim Jong Un |
Imeelezwa kuwa wananchi wa taifa hilo wanaokadiriwa kufikia 800,000 wameonesha utayari wa kujiandikisha na kulitumikia Jeshi la Taifa ili kukabiliana na Marekani, Gazeti la Serikali la Korea Kaskazini Rodong Sinmun limeripoti taarifa hiyo.
Baadhi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini |
Madai hayo yamekuja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora la Hwasong-17 (ICBM) ikiwa ni hatua ya kujibu mapigo ya mazoezi ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini yanayoendelea.
Makombora ya aina ya ICBM ya Korea Kaskazini yamepigwa marufuku chini ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na zoezi hilo lililaaniwa na Serikali za Korea Kusini, Marekani na Japan.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekuwa akiishutumu Marekani na Korea Kusini kwa kuongeza mvutano baina yao kwa kitendo cha wao kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi.
0 Comments