![]() |
| Nembo ya Yanga |
“Kwa sasa hivi niwahakikishie wale waliokuwa wakitania jana, niliona utani nampigia Msigwa namwambia ‘ebu maliza mpira haraka mimi pesa zimeisha’, nataka niwahakikishie kwamba Mama bado anazo wekeni mipira kwenye wavu jengeni jina la Nchi yetu, bado zipo,”amesema Rais Dkt. Samia.
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema bado zile milioni tanotano za kununua magoli ya Simba na Yanga kwenye mechi za kimataifa zipo, ameyasema leo akiwa Dar es salaam katika Sherehe za maadhimisho ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).
![]() |
| Mchezaji wa simba, Chama |
“...niliona utani nampigia Msigwa hembu maliza mpira haraka mimi pesa zimeisha, nataka niwahakikishie kwamba mama bado anazo, wekeni mipira kwenye wavu, jengeni jina la nchi yetu".


0 Comments