Ticker

7/recent/ticker-posts

MIAKA MIWILI YA MARIDHIANO, USTAHAMILIVU

  

Rais Dkt. Samia akiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
KATIKA kipindi chake cha uongozi ambacho kimetimiza miaka miwili leo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na kumaliza janga la Uviko-19 kwa kutumia njia za kisayansi.

 

Kuwarejesha wawekezaji wa nje na kufufua uwekezaji wa ndani

Ameimarisha sera ya mambo ya nje na uhusiano wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa

 

Amerejesha uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza, asasi zisizo za kiserikaki, maridhiano ya kisiasa na kufuta marufuku ya mikutano ya kisiasa


Ujenzi wa Bwawa la Nyerere unaendelea
Ameonesha Shamir ya kufufua mchakato wa kupata katiba mpya, ameongeza bajeti ya kilimo kwa mara nne, amevunja rekodi ya uwekezaji kwenye afya, elimu na miradi ya maji

Ameongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati, ikiwemo SGR, JNHPP, ununuzi wa ndege za ATCL na ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi

 

 Amefufua mazungumzo na wawekezaji wa nje kwenye mradi wa LNG wa Shilingi trilioni 93 wa kuchakata gesi, ameanzisha mchakato wa kuimarisha haki jinai nchini

Amebadilisha mwelekeo wa nchi kutoka kwenye siasa za uhasama na kuhamia kwenye siasa za staha na maridhiano

Post a Comment

0 Comments