Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS DK.MWINYI ATAKA CHANGAMOTO ZA BIASHARA ZITATULIWE

 


Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZNBC) , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amezitaka Wizara na wadau wa sekta mbalimbali zinazofanya biashara wakutane kila miezi mitatu kujadiliana kuhusu changamoto na kuzipatia ufumbuzi. 

 

Pia amelitaka Baraza la Biashara la Taifa kukutana kila baada ya miezi sita  huku Jukwaa likutane mara moja kwa Mwaka katika kuongeza ufanisi zaidi kwa utatuzi wa changamoto  za biashara nchini. 

 

Aliyasema hayo alipofungua Jukwaa la 12 la biashara leo tarehe 19 Machi , 2023 lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, visiwani hapa. 


Aidha , Dk.Mwinyi amegusia  maazimio ya Baraza hilo ikiwemo masuala ya kodi na kuwataka Wizara ya Fedha ,TRA  na ZRA wakutane na kujadiliana namna ya  kuyatatua huku wakipeleka taarifa  za utatuzi  wa changamoto hizo katika jukwaa . 

Vilevile,  alieleza kuwa Serikali ipo   kwa ajili ya kutatua changamoto..

Post a Comment

0 Comments