![]() |
| Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda |
Hatua hiyo inalifanya jeshi hilo kuwatoa hofu wananchi hasa wanaoishi katika mpaka wa Tanzania na Malawi kwani zoezi la kupeleka msaada kwa majirani hao litahusisha msafara wa magari mengi ya kijeshi ambayo yatakuwa yanavuka mpaka kuelekea huko.
Akitoa taarifa hiyo jijini Dodoma, Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema serikali kupitia jeshi la ulinzi inapeleka msaada nchini Malawi kutokana na kupata tatizo la kimbunga Fredy.
Misaada inayopelekwa Malawi inahusisha vyakula, mahema na misaada mingine ya kibinadamu.
Juzi Luteni Kanali Ilonda alisema "Kufuatia maafa ya kimbunga nchini Malawi, Serikali imeamua kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ili kuisaidia nchi jirani, JWTZ imepewa jukumu la kusafirisha misaada hiyo.
"Tunatarajia shehena zitaondoka muda wowote kuanzia sasa, jumla ya tani 1,000 za unga wa mahindi zitasafirishwa kwenda Malawi, amesema tani 90 zitaondoka kila siku zikitokea Dodoma.
"Tani 60 za unga zitaondoka kila siku kutokea mkoani Iringa, mablanketi 6,000 yataondokea yakitokea Dodoma, mahema yasiyopungua 50 yataondoka yakitokea jijini Dar es Salaam," ameeleza Luteni Kanali Ilonda.

0 Comments