Ticker

7/recent/ticker-posts

MATAIFA MANNE AFRIKA YATISHIA MAANDAMANO

 

Kiongozi wa Muungano wa Azimio, Raila Odinga akiwa na wafuasi wake
LEO nchi nne za Afrika zimetishia kufanya maandamano yasiyo na kikomo kwa hoja mbalimbali, nchini Kenya, baadhi ya raia wan chi hiyo wanaouunga mkono upinzani wanajiandaa kwa maandamano yaliyoitishwa na kinara wa muungano wa upinzani wa Azimio, Raila Odinga, ambaye anapinga kupanda kwa gharama za maisha na utawala wa rais William Ruto.

 Jana  Odinga alisisitiza kuwa maandamano ya hivi leo yako pale pale licha ya katazo la polisi kwenye jiji la Nairobi.

 

Kwa upande wake Rais Ruto, tayari amewaonya wale aliosema watu wanaopanga kusababisha vurugu nchini humo, na kwamba serikali yake haitawavumilia wavunjifu wa amani, akimtaka Odinga kuachana na mpango wake.

Nchini Nigeria, kwenye mji wa Lagos wanasiasa wa upinzani wameitisha maandamano ya kuonesha msisitizo wao wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita.

Mjini Tunis,yamepangwa maandamano ya kupinga utawala wa kiimla wa rais Kais Saied wa nchi ya Tunisia, waandamanaji wa upinzani wamekuwa wakikusanyika mjini Tunis.

Kiongozi wa chama cha EFF, Julius Malema
Nchini Afrika Kusini,kiongozi wa chama cha EFF Julius Malema ametishia kuongoza maandamano makubwa zaidi yatakayolitikisa taifa hilo,tayari wameifahamisha serikali kuwa hawataomba ridhaa ya kuandamana.

Senegal, kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na wafuasi wake wamepanga kuandamana mjini Dakar kupinga azma ya rais aliyeko madarakani Macky Sall kuwania muhula wa tatu unaozua utata.

Post a Comment

0 Comments