Katika kuhakikisha kila binadamu anakuwa na furaha Umoja wa Mataifa uliitangaza Machi 20 ya kila mwaka kuwa siku ya furaha duniani ikiwa na nia ya kuwakumbusha watu umuhimu wa kufurahi na kufurahia kila hatua ya maisha.
Siku hii inatukumbusha kutambua umuhimu wa kuhakikisha ukuaji wa uchumi unasaidia kuleta maendeleo endelevu, kutokomeza umaskini na kuleta furaha kwa jamii.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022, Finland ndiyo nchi ambayo wananchi wake wanafuraha zaidi duniani na barani Afrika Mauritius ndiyo inayoongoza.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika Siku ya furaha ni :Kuwa mtu makini, kuwa mtu mwenye kushukuru na uwe mkarimu kwa wenzio.
0 Comments