Ticker

7/recent/ticker-posts

‘DHAMANA POLISI NI BURE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo 
LIMEKUWA ni jambo la kawaida kwa watu wengi kusema kuwa ni bure kuingia katika kituo chochote cha Polisi pale unaposhtakiwa na kuwekwa mahabusu, lakini hali inakuwa tofauti unapotaka kutoka ni lazima ulipe chochote pale unapohitaji kupata dhamana hata kama una haki ya kudhaminiwa.

 

Mwenendo huo umekuwa ukitazamwa kama kitega uchumi cha baadhi ya askari kwenye vituo mbalimbali vya polisi, aidha tabia hiyo inatajwa kuondoa haki ya msingi ya mtuhumiwa.

 

Katika harakati ya kulikomesha suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku utaratibu wa watuhumiwa kutozwa pesa pindi wanapohitaji dhamana, kwani hiyo ni haki yao kisheria.

 

Kauli hiyo ya RPC Jongo, inaweza kusaidia kuondoa urasimu kwenye suala la kupatiwa dhamana kwa watuhumiwa.

 

Post a Comment

0 Comments