Ticker

7/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIPONGEZA PSSSF KWA KUWAFIKIA WANANCHI


Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, tuzo kwa ajili ya kufanikisha sherehe za miaka 10 ya e-GA 


Na Mwandishi Wetu, Arusha 

SERIKALI imeupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF) kwa kuwafikia wananchi wengi nchini. 

 Pongezi hizo zimetolewa jijini Arusha na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi katika hotuba yake ya ufunguzi wa sherehe za kutimiza miaka 10 ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao, kinachokutanisha wataalam wa TEHAMA kutoka serikalini PSSF imefanikisha suala hilo la kuwafikia wananchi kwa urahisi kutokana na kutumia vizuri Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

 “Nimejionea kwenye mabanda, PSSSF wameweza kuweka App ili kuweza kuona michango inavyokwenda, nielekeze e-GA kuendelea kufanya tafiti ili kuleta bunifu za mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta za viwanda, biashara na uwekezaji ili kulipeleka taifa mbele kimaendeleo,” alisema Mhe. Ndejembi. 


Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Peter Ulanga, akiwa kenye picha ya pamoja na watumishi wa PSSF alipotembelea  banda la PSSSF katika kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao, AICC Arusha.

Aidha Ndejembi amezishauri taasisi nyingine za umma kuitumia TEHAMA ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za serikali kwa haraka. 

Matumizi ya TEHAMA yamekuwa na manufaa makubwa kwa PSSSF ambayo sasa inatoa huduma zake kwa njia ya PSSSF Kiganjani na PSSSF Mtandaon. Huduma hizi zimesaidia kuwapunguzia urasimu wanachama wao pamoja na kuwaondolea adha ya kufunga safari ili kwenda kwenye ofisi za mfuko huo.
Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Deogratius Ndejembi (wa nne kutoka kushoto) akipokea kitabu cha Mwongozo kwa Mwanachama kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (wa pili kushoto), wakati alipotembelea banda la PSSSF katika Maadhimisho ya miaka kumi ya e-GA, jijini Arusha. 


Post a Comment

0 Comments