Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AENDELEA KUPANGA SAFU YA UONGOZI


Rais Samia Suluhu Hassan


BAADA ya hivi karibuni kuteua na kutengua wakuu wa wilaya mbalimbali nchini, leo Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kupanga safu yake ya uongozi kwenye taasisi za umma kwa kumteua Ndugu Ephraim Mafuru kuwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Ndg.Ephraim Mafuru
Kabla ya uteuzi huo Mafuru ambaye amehudumu kwenye maeneo mbalimbali, alikuwa ni Mkuu wa Masuala ya biashara kwenye kiwanda cha Sukari Kilombero, mkoani Morogoro.

 Uteuzi wa Mafuru umeanza jana Februari 9,20223. 




Post a Comment

0 Comments