Tundu Lissu akilakiwa na wafuasi wa Chadema mara baada ya kuwasili nchini jana |
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara Tundu Lissu, amabaye amerejea nchini jana, amewataka wanachama wa chama hicho kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye masuala mbalimbali yenye maslahi ya Taifa.
Lissu ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara kwenye uwanja wa Buliaga wilayani Temeke, Dar es Salaam aliofanya mara baada ya kurejea nchini akitokea Ubelgiji.
Amesema CHADEMA ina kazi kubwa ya kuhamasisha watanzania kuhusu maboresho ya sheria zilizopitwa na wakati , Ili kuendana na mazingira yaliyopo sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amewataka wadau wote wa siasa kushirikiana katika kuisimamia serikali ili iweze kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya.
0 Comments