Ticker

7/recent/ticker-posts

BARAZA LA MITIHANI LAACHA KUZITANGAZIA SHULE DILI, LAONDOA UTARATIBU WA 10 BORA

 


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne (CSEE) na Maarifa (QT) iliyofanyika Novemba 14- Desemba 1, 2022 nchini kote.

 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,  Athuman Amasi ndie aliyetangaza matokeo hayo leo Jumapili Januari 29,2023 kwenye makao makuu ya NECTA, jijini Dar es Salaam.


Aidha Amasi alisema Baraza pia limeondoa utaratibu wa kutangaza  shule 10 bora na watahiniwa 10 bora kwa sababu mfumo huo hauna tija kwa nchi.


Alisema hatua hiyo imefikiwa kwa sababu hakuna usawa kuwafananisha watu wanaofanya mitihani kwenye mazingira tofauti ingawa mitihani unafanana.


"Tulizoea kusikia lugha za top 10, wasichana wawagaragaza wanaume, sasa tuondoke kwenye mazoea hayo, ukigundua jambo unalolifanya halina tija huna haja ya kuendelea nalo, unamtaja mtu ameongoza na kumlinganisha na watu ambao hawakusoma katika mazingira yaliyofanana sio sawa.


"Kama kuna shule ilikuwa inasubiri itangazwe kuwa Top 10 hiyo haipo, kwanza kutangaza shule ya kwanza huenda tulikuwa tunawafanyia marketing (Kuwatafutia soko) na ndio maana tumeona haina tija."



MATOKEO YOTE...

www.nacte.co.tz

Post a Comment

0 Comments