KLABU ya michezo ya Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo imempoteza mwanachama na kiongozi wake wa zamani Said Rubeya.
Wakati wa uhai wake Rubeya mbali ya kuwa mwanachama mwandamizi wa klabu hiyo, lakini pia aliwahi kushikilia wadhifa wa Katibu Mwenezi.
Said Rubeya wakati wa uhai wake (Picha kwa hisani ya Kitenge Tv) |
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, mtoto wa Rubeya, Aristide Rubeya alisema baba yake alifariki usiku wa kuamkia leo na wanatarajia kuupumzisha mwili wake jioni ya leo kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Rubeya alikuwa akiishi Kariakoo mtaa wa Tandamti na Msimbazi (Masjid Idrissa) na hapo ndipo msiba wake ulipo.
0 Comments