Ticker

7/recent/ticker-posts

DIRA 2050 IMEKAMILIKA, RAIS DKT. SAMIA KUIZINDUA JULAI 17,DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi DIRA 2050 Julai 17, 2025, iliyobeba kaulimbiu ya "Tanzania Tuitakayo 2050".

Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari mbalimbali, jijini Dar es Salaam, leo Julai 18,2025, Prof. Kitila amesema uzinduzi huo utafanyika baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuiandaa dira hiyo ulioanza Mwaka 2023.

Amesema maandalizi ya Dira hiyo yalihusisha maoni kutoka kwa wananchi, wadau wa maendeleo na wasomi zaidi ya milioni 1.1 nchi nzima.

 ushirikishwaji wa wananchi 

Kaya zaidi ya 15,000 zilifikiwa na maoni zaidi milioni 1.1 yaliwasilishwa kwa njia ya ujumbe mfupi.

Viongozi 44 waliopo madarakani na waliostaafu walifikiwa na kutoa maoni yao na makongamano 12 yalifanyika.

Prof. Kitila amesisitiza kuwa watekelezaji wakuu wa DIRA 2050 unawalenga zaidi vijana wa sasa kwa sababu wao ndio watakuwa na umri wa utu uzima hadi kufikia mwaka 2050.

Akiongelea ulinzi wa Dira hiyo, Prof. Kitila amesema hatua ya kupitishwa na Bunge inatosha kuilinda na kwamba hakuna kiongozo yeyote ambae ataweza kutoitekeleza bila kupata ridhaa ya Bunge.

"Hii dira inaweza kutekelezwa na marais watatu au zaidi tofauti, kwa kulizingatia hilo tumeiwekea ulinzi wa Bunge, hakuna kiongozi yeyote atakaeweza kuibadilisha kwa matakwa yake."

Prof. Kitila amesema kabla ya uandaaji wa DIRA hiyo wataalmu wa serikali walifanya utafiti katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na katika nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kama Botswana, Singapore, Morocco, Afrika Kusini na mataifa mengine ya Asia Mashariki na baadhi ya nchi za ulaya na utekelezaji wake utaanza rasmi Julai 1, 2026.

Post a Comment

0 Comments