Ticker

7/recent/ticker-posts

KCB YAWEZESHA VIJANA 2185 KUJIAJIRI, YAWAPA NAFASI VIJANA KUJITANGAZA SABASABA


 Vijana wajasiriamali waliowezeshwa na Benki ya KCB Tanzania, wakiwa kwenye maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea, jijini Dar es Salaam.

 NA MWANDISHI WETU

 

Benki ya KCB Tanzania, imefanikiwa kuwawezesha vijana 2185 kujiajiri, baada ya kuwasadia kupata mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali. Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa benki hiyo Khadija Miraji Mjatta, kwenye maonesho ya kimataifa ya 48 ya Sabasaba yanayoendelea, jijini Dar es Salaam.

 

Mjatta amesema KCB Tanzania ni mdau mkubwa wa maendeleo kwa miaka 25 sasa na wamekuwa wakitoa huduma masuala ya kifedha kupitia huduma bora na nafuu.

 

Amesema wako kwenye maonesho hayo ya sabasaba kwa ajili ya kuionesha jamii juu ya program yao ya Tujiajiri ambayo imekuwa ikiwawezesha vijana wa kike na kiume kwa kuwasomesha na kuwaendeleza kwenye fani mbalimbali.

 

 Meneja Uhusiano wa benki ya KCB Tanzania Khadija Miraji Mjata, 


“Kupitia program hii tumewanufaisha vijana 2185, kati yao wanaume 1117 na wanawake 1168 ambao wote wanajihusisha na masuala ya ujasiriamali na KCB imekuwa ikiwaendeleza kimasomo kwenye vyuo mbalimbali nchini.

 

“Tunao vijana wengi ambao wameingia kwenye mchakato wa kuwania nafasi hizo za kuendelezwa.”

Alisema vijana wanaowezeshwa na KCB wanajihusisha na utengenezaji wa batiki, sabuni,ushonaji na  usindikaji wa vyakula.

 

KCB imewapa banda kwenye maonesha ya 48 ya sabasaba ili waoneshe ujuzi wao baada ya kupatiwa mafunzo.

“Vijana walikuwa wengi lakini ni vijana sita ndio wamefanikiwa kushinda kwenye mchakato wa kupata nafasi ya kupewa banda kwenye manesho hayo ya sabasaba.

 

“Natoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi zaidi hasa pale program ya Tujiajiri inapotangazwa na wasiogope kukimbilia fursa zinapojitokeza popote pale,”alisema Mjatta.



Post a Comment

0 Comments