Ticker

7/recent/ticker-posts

HALI NI SHWARI RUFIJI, ASKARI WA TAWA WAENDELEA KUFANYA DORIA SAA 24


NA JIMMY KIANGO

Ile hofu ya  kuwapo kwa mamba na viboko waliodaiwa kuzagaa kwenye makazi ya watu, wilayani Rufiji mkoani Pwani halipo tena baada ya askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuimarisha ulinzi kwa saa 24 kwenye maeneo yote hatarishi.

 

Awali kulikuwa na tishio la mamba na viboko kuingia kwenye baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko wilayani Rufiji. Hata hivyo haraka TAWA ilipeleka kikosi maalum cha doria wilayani humo zanjar na kutoa elimu ya namna ya kuepukana na hater itakayoweza kusababishwa na wanyama hao.


Hatua hiyo ya TAWA kuimarisha ulinzi ilisaidia kuwaruhusu wavuvi kuendelea na shughuli zao za uvuvi kwenye mto Lugongwe. ikumbukwe kuwa shughuli za kilimo na uvuvi ndizo zinazowaingizia kipato wakazi wa Kata ya Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani na wamekuwa wakiutumia mto Lugongwe kuendesha shughuli zao hizo.

 

Tangu kutokea kwa mafuriko wilayani humo kumekuwa na tishio la kuongezeka kwa mamba na viboko kwenye mto huo hali iliyowafanya wavuvi wengi kusitisha shughuli zao.

Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja.

                                      

Akizungumza na AFRINEWSSWAHILI, hive karibuni Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja alisema kwa sasa hali ya usalama ni nzuri sana na imeimarishwa vya kutosha. “Askari wanafanya doria muda wote wakihakikisha wanalinda maisha ya binadamu, TAWA hatuko tayari kuona binadamu wanadhuriwa na wanyamapori hasa mamba.

 

“Lakini pia kama tulivyoeleza awali, elimu ya namna ya kujiepusha na hatari ya wanyamapori hao inaendelea kutolewa na hii inatusaidia kurahisisha kazi yetu, kwani wananchi wanajua nini cha kufanya na nini wasifanye.

“Pamoja na mambo yote hayo, bado askari wa TAWA wanaendelea na msako wa mamba, na tutahakikisha hakuna binadamu anaedhuriwa na wanyamapori na kwa sasa hali ni shwari kabisa katika maeneo yote,”alisema Maganja.

Maganja alisema ni jambo la fedheha kwa TAWA kuona binadamu wanakufa kwa sababu ya kuuliwa na mamba, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha binadamu wanakuwa salama na shughuli zao zinaendelea kama kawaida.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments