Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) CP Salum Hamduni. |
NA MWANDISHI WETU-AFRINEWSSWAHILI-DODOMA
Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) CP Salum Hamduni amesema uchunguzi uliofanywa na taasisi yake umebaini kuweo kwa mianya ya rushwa kwenye miradi 12 ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.
CP Hamduni ameyasema hay oleo Machi 28,2024 kwenye Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa mwaka 2022/23 mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Mheshimiwa Rais katika kutimiza majukumu yake TAKUKURU imefuatulia pia miradi 12 ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji yenye thamani ya shilingi bilioni 107.4 katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Tabora na Mbeya, matokeo ya ufuatiliiaji yalionesha uwepo wa mianya ya Rushwa, baadhi ya miradi ilionekana kutosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (BUW) na wakala wa usalama mahala pa kazi, ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi uliosababisha uwepo wa riba, malipo kufanyika pasipo baadhi ya kazi kufanyika, malighafi za ujenzi kutopimwa ubora wake kinyume na mikataba, ujenzi kufanyika kinyume na matakwa ya mkataba, kutozingatiwa kwa sheria na kanuni za ununuzi wa umma na pia kuwepo kwa nyongeza ya kazi au variation pasipo kufuata utaratibu" -CP Hamduni
"Kutokana na matokeo ya ufuatiliiaji TAKUKURU ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhakikisha kuwa marekebisho kwenye miradi husika inafanyika na tulilenga zaidi kuhakikisha kwamba serikali haipati hasara, kutoa elimu kwa wasimamizi wa miradi, pamoja na kushauri mamlaka zilizohusika namna bora ya kuziba mianya ya Rushwa ambayo ilibainika
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni amezungumza hayo wakati akiwasilisha ripoti ya taasisi hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
0 Comments