Ticker

7/recent/ticker-posts

'MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA,OFISI YA MSAJILI WA HAZINA IMEONGEZA THAMANI YA UWEKEZAJI’

 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

NA JIMMY KIANGO-AFRINEWSSWAHILI-DSM

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ameimwagia sifa ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kuongeza thamani ya uwekezaji katika taasisi zinazosimamiwa na ofisi hiyo.

Matinyi amemwaga sifa hizo jana Machi 24,2024 jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari wakati wa kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alisema thamani ya uwekezaji katika taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina imeongezeka kutoka shilingi trilioni 70 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi trilioni 76 mwaka 2023 – sawa na ongezeko la 8.6%.

Sababu ya ongezeko hili ni Serikali ya Awamu ya Sita kuongeza mitaji kwa kiasi cha shilingi trilioni 5.5 katika mashirika yakimkakati kwa maslahi ya taifa.


“Ofisi pia imeongeza makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kutoka shilingi bilioni 637.66 hadi trilioni 1.008 kwa mwaka 2023, sawa na ongezeko la 58%. Serikali pia imeongeza umiliki wa hisa katika kampuni ya almasi ya Williamson Diamonds kutoka 25% hadi 37% hukuikisaini mikataba ya ubia wa 16% zisizohamishika katika kampuni za madin,” alisema Matinyi.

Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu.

MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA MADINI 

Kwenye eneo la madini, Matinyi alisema katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi 2021 hadi Februari 2024 Wizara ya Madiniimefanikiwa kuiendeleza sekta kwa namna mbalimbali ikiwemo kukusanya maduhuli yatokanayo na ada mbalimbali,mirabaha, faini na penati na kufikisha kiasi cha shilingi trilioni

1.93. Awali mwaka 2021/22 ilikuwa shilingi bilioni 591.5 lakini hadi kufikia mwaka 2023/24 imefikia shilingi bilioni 690.4.

 

Aidha, katika kipindi cha Machi 2021 hadi Februari 2022 mauzo ya madini mbalimbali yalikuwa shilingi bilioni 157.34 lakini kufikia kipindi cha Machi 2023 hadi Februari 2024 mauzo yamefikia shilingi bilioni 476.8.

 

KILIMO KINAELEKEA KUWA NA TIJA KUSUDIWA

Kwenye kilimo bajeti imeongezeka kutoka shilingi bilioni 294.16 mwaka 2021/2022 hadi kufikia shilingi bilioni shilingi bilioni970.78 mwaka wa fedha 2023/2024.

 

Mkurugenzi wa Idaya ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi.


Matumizi ya mbolea yameongezeka kutoka tani 320,233 kwa mwaka wa fedha 2020/21 hadi kufikia tani 580,628 kwa mwakawa fedha 2022/23.

 

Bajeti ya maendeleo ya umwagiliaji imeongezeka kutoka shilingi bilioni 46.5 mwaka 2021/22 hadi shilingi bilioni 361.5 mwaka 2023/24 ambapo wataalam wa kilimo 320 wameajiriwa na kusambazwa katika ofisi za umwagiliajizilizopo katika wilaya 139.

 

Mitambo 15 na magari 53 vimenunuliwa kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji, eneo la umwagiliaji limeongezeka kutoka hekta 694,715 mwaka 2020/2021 hadi hekta 727,280.6 mwaka 2022/2023. 

 

Serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa skimu za umwagiliaji zenye hekta 95,000 zilizoanza mwaka 2022/2023pamoja na kuanza skimu mpya zenye ukubwa hekta 95,000 kwa mwaka 2023/2024, ambapo kukamilika kwake kutaongeza eneo la umwagiliaji kufikia hekta 917,280.

 

Programu ya Vijana ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Build Better Tomorrow-BBT). Mradi unashirikisha vijana 688, ambaowameanza kilimo biashara katika shamba la Chinangali II.

 

Post a Comment

0 Comments