Ticker

7/recent/ticker-posts

POLISI, DCPC KUMLINDA MWANDISHI WA HABARI AWAPO KAZINI

  

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Jumanne Muliro

NA MWANDISHI WETU-AFRINEWSSWAHILI-DSM

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum (Dar es Salaam) na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) na wameunda Kamati ndogo kwa ajili ya kusimamia na kufuatilia ulinzi na usalama wa waandishi wa habari wanapokuwa kazini

 

Kamati hiyo yenye wajumbe sita imeundwa Machi 22, kwenye mdahalo wa majuisho kati ya DCPC na Jeshi la Polisi. Wajumbe wa Kamati hiyo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Malulu, ambaye pia ni RPC wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Askofu Emaus Mwamakula na Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Adam Mwinyipingu.

 

Wengine ni Wakili Mkumbo Emmanuel, Katibu Mkuu wa DCPC, Fatuma Jalala na Bakari Kimwanga (mwanachama wa DCPC). Kuundwa kwa Kamati hiyo ni matokeo ya midahalo mitatu kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari, pamoja na kusimamia haki na sheria. 

 

Mwenyekiti wa DCPC, Samson Kamalamo .

Midahalo hiyo iliyoanza Novemba 2023 na kumalizima Februari  2024, iliratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kudhaminiwa na shirika la IMS, ilihusisha Kanda Maalum (Ilala ikiwemo), Temeke na Kinondoni, ambapo maazimio kadhaa ya kiutendaji yalifikiwa.

 

Miongoni kwa maazimio hayo ni kuwepo kwa mabonanza ya kimichezo kwa lengo la kujenga ukaribu, kuhakikisha usalama wa waandishi wanapokuwa kazini na hata katika operesheni za polisi, kuwepo kwa kanzidata ya waandishi wa habari ambayo itatambuliwa na polisi, lakini pia Polisi kufanya kazi kwa karibu zaidi na uongozi wa DCPC.

 

Awali akimkaribisha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Jumanne Muliro, Mwenyekiti wa DCPC, Samson Kamalamo alisema , ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya Polisi na Waandishi wa habari umefunguliwa.

 

Amesema ushirikiano huo unakwenda kuhakikisha ulinzi na usalama wa waandishi wa habari, pia kuwaepusha polisi dhidi ya maumivu yanayosababishwa na kalamu. Kamanda Muliro ameahidi kuwa polisi itaendelea kusimamia haki kama vile zinavyotambuliwa  kitaifa na kimataifa na kwamba anawahakikishia waandishi wa habari kuwa salama.

Wajumbe walioshiriki kwenye mdahalo wa majuisho kati ya DCPC na Jeshi la Polisi.


Post a Comment

0 Comments