Ticker

7/recent/ticker-posts

MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA IMEJAA MAFANIKIO NDANI YA TFS, DARASA LA KUBAINI ASALI FEKI LATOLEWA

 

Mtendaji Mkuu wa TFS,Profesa Dos Santos Silayo 

NA JIMMY KIANGO-AFRINEWSSWAHILI-DAR ES ASAALA

 

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) leo Machi 19,2024 imeadhimisha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu, madarakani kwa kuanisha mafanikio waliyoyafikia katika kipindi cha miaka mitatu, ikiwa ni pamoja na kutoa darasa la namna ya kuijua asali feki.

 

Mafanikio hayo yameelezwa mbele ya Wahariri na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya Habari Tanzania na Mtendaji Mkuu wa TFS,Profesa Dos Santos Silayo katika muendelezo wa vikao kazi vilivyoandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina.

 

Profesa Silayo alitoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia ya kuongoza nchi vizuri pamoja na kuboresha sekta ya Maliasili na Utalii.

 

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia, TFS imeweza kutekeleza shughuli mbalimbali kwa mafanikio makubwa ikiwemo kusimamia rasilimali watu, rasilimali za misitu, uendelezaji wa mashamba ya miti ya serikali, utalii, ikolojia na utamaduni na ufugaji nyuki.

Baadhi ya Wahariri na Waandishi waliohudhuria mkutano huo.

 Mengine ni ukusanyaji wa maduhuli na mchango kwenye mfuko mkuu, maendeleo ya viwanda na biashara, utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuimarisha mazingira ya kazi, kushirikisha wadau katika uhifadhi, utalii na elimu kwa umma, huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya Taifa.

 

Kwenye eneo la usimamizi wa rasilimali watu mamlaka hiyo inasimamia maofisa 643 na askari 1,454, ambapo katika kipindi cha mwaka 2020/2021-2023/24 mamlaka iliajiri watumishi wapya 495, ambapo watumishi 180 walipatiwa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 1,481, walipatiwa mafunzo ya muda mfupi.

 

Aidha katika kipindi hicho juhudi za Rais Samia zimesaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea vituo vya utalii ikolojia kutoka 59,606 mwaka 2020/21 hadi 242,824 mwaka 2022/23.

 

Ongezeko hilo la watalii limesaidia kuongeza mapato kutoka shilingi 154,965,050 hadi kufikia wastani wa shilingi 1,5018,940,965, ambayo ni mafanikio maiubwa yaliyowahi kupatikana na wakala katika sekta ya utalii eneo la ikolojia kuliko wakati mwengine wowote. Hayo ni baadhi ya mafanikio mengi yaliyofikiwa na TFS ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Ofisa kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa TFS na Wahariri na Waandishi.

KUIJUA ASALI FEKI

Prof. Silayo ametoa darasa dogo kwa Watanzania kuitambua asali halisi na ile feki, ambapo amesema ili kuijua asali feki mwananchi anapaswa kutumia njiti ya kibiriti au karatasi lolote lile kubaini.

 

“Chukua njiti ya kiberiti, kisha ichovye kwenye asali, baada ya hapo iwashe hiyo njto kwa kutumia kiberiti, kama njiti itawaka basi hiyo asali uliyonunua ni halisi kwa sababu njiti itakuwa kavu na kama njiti haitawaka na itakuwa imelowa basi hiyo ni feki.”

 

Kuhusu kuitambua asali feki na halisi kwa kutumia karatasi, alisema mwananchi anapaswa kuimwaga kidogo asali kwenye karatasi, kama karatasi litalowa hadi upande wa pili kama iliyomwagiwa maji, basi hiyo asali ni feki na kama halitalowa basi ni halisi.

 

Amaesem mtu anayehitaji asali halisi anapaswa kuinunua kwenye maduka ya TFS,ambayo yapo katika maeneo mengi ya nchi.

 

Post a Comment

0 Comments