Ticker

7/recent/ticker-posts

ALEX MSAMA ATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI

MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama 

NA MWANDISHI WETU-AFRINEWSSWAHILI-DSM

Siku chache baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa kumtaka MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kufika kwa Kamishna wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam, hatimae mfanyabiashara huyo ametekeleza agizo hilo jana Machi 28,2024.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Machi 29,2024 Msama amesema alienda ofisini kwa Kamishina wa Ardhi na kueleza kuwa kuna maelekezo amepewa atayafanya na kwa vile jambo hilo tayari lipo wizarani basi litafanyiwa kazi. 

Katika mazungumzo yake hayo Msama alimsifia Waziri Silaa kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema kuwa wizara hiyo imepata mchapa kazi.

 

“Waziri wetu ni mtu anayefanya kazi yake vizuri sana na hakika Wizara ya Ardhi imempata mchapa kazi mzuri, nampongeza. - “Lakini nimeona pia nitoe pia ufafanuzi zaidi kuhusu kiwanja kinachozungumziwa kilichopo Kibada wilayani Kigamboni, kiwanja hicho chenye namba DSMT 1022673 sijakivamia ni changu na nakimiliki kihalali. - “Sijawahi kumtapeli mtu kiwanja, nina nyaraka zote za umiliki, nimemilikishwa na Wizara ya Ardhi. 

 

Kuhusu kuwa na kiwanja eneo la Mbweni, hicho sikitambui na si changu,” amesema Msama. 

Post a Comment

0 Comments