Kichapo cha bao 5-1 ilichokipata tiku ya Simba kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kimesababisha kutimuliwa kwa kocha wa timu hiyo Roberto Oliveira maarufu kama Robetinho.
Uamuzi huo umetolewa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Imani Kajula.
Simba sasa inamsaka mrithi wa Robetinho hata hivyo kwa sasa timu itakuwa chini ya Daniel Cadena na Sulaiman Matola.
Robetinho ametimuliwa sambamba na kocha wa viungo Comeille Hatagekimana.
0 Comments