Shirikisho la Soka Africa (CAF) limetangaza rasmi kuwa, VISIT SAUDI ndio wadhamini wakuu wapya wa michuano mipya ya African Football League ambayo inatarajia kuzinduliwa Oktoba 20, 2023, jijini Dar es Salaam na kuisha Novemba 11, 2023.
Timu zinazo shiriki michunaonhiyo ni Al Ahly, Wydad, Esperance, Mamelodi, Simba, Petro de Luanda, TP Mazembe na Enyimba na zote zimepewa dola 1,000,000 ambayo zaidi ya bilioni shilingi 2.5.
Fedha hizo ni kwa ajili ya ushiriki kuanzaia hatua ya robo Fainali na iwapo timu itafuzu hatua ya nusu fainali itapata ongezeko la dola 700,000 (shilingi bilioni 1.75)
Timu ikiwa bingwa wa mashindano ya African Football League 2023 itapata ongezeko la dola 2,300,000 (bilioni 5.75) kutoka nusu fainali na kuwa na jumla ya dola 4,000,000 (bilioni 10) huku mshindi wa pili atapata ongezeko la dola 1,300,000 (bilioni 3.25) na kuwa na jumla ya dola 3,000,000 (bilioni 7.5).
0 Comments