Ticker

7/recent/ticker-posts

VISION PLUS YAPEWA TUZO YA MTEJA BORA WA LENZI ZA MIWANI JAPAN

Ndugu Datoo (kushoto) akiwa na Bwa. Furuzawa.

Kituo cha Vision Plus Tanzania kinachotoa huduma ya afya ya macho na miwani leo Oktoba 18,2023 kimepewa tuzo maalum ya kimataifa ya mteja bora wa Lenzi za miwani.

Tuzo hiyo imetolewa na  kampuni ya TOKAI yenye makao makuu yake nchini Japan.

Mkurugenzi wa TOKAI LENSES, Bw. Hirokazu Furuzawa ndie aliyetoa tuzo hiyo kwa Vision Plus.

Akizungumzia tuzo hiyo mtaalam bingwa wa macho nchini Tanzania, ambaye pia ni mmiliki wa kituo bora cha kutoa huduma za macho cha Vision Plus, Ndugu. Husseinali Datoo, alisema wamefurahishwa na tuzo hiyo na wataendelea kufanya biashara na TOKAI.

Ndugu Dattoo alisema Vision plus ndiye mteja bora zaidi wa lenzi za TOKAI katika ukanda wa  Afrika Mashariki.


Tuzo ya mteja bora iliyotolewa kwa Vision Plus.


Ndugu Datoo 

Post a Comment

0 Comments