Ticker

7/recent/ticker-posts

ADHABU YA TFF YAMPA SOMO MSEMAJI WA YANGA

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema amepokea adhabu ya kulipa kiasi cha shilingi milioni moja aliyopewa na Bodi ya Ligi ya  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama darasa kwake.

Amesema adhabu  hiyo ni kama njia ya Mungu kutaka kuzungumza naye, kwani kupitia adhabu hiyo ameona, kusikia na kujifunza mengi na kikubwa ameuona upendo wa dhati wa mashabiki wa Yanga kwake na amewashukuru kwa kuweza kumchangia kiasi hicho cha pesa.

Tayari muda mfupi baada ya Ali kamwe kupigwa faini hiyo kwa kosa la kumkejeli mwamuzi Tatu Malogo kupitia mitandao ya kijamii, mashabiki wa Klabu hiyo wamejichanga na kupata kiasi hicho kupitia kampeni iliyoendeshwa na shabiki Jimmy Kindoki ili kumuwezesha kulipa faini hiyo kwa wakati na kuendelea na majukumu yake.



Post a Comment

0 Comments