Ticker

7/recent/ticker-posts

MCHEKESHAJI WA NIGERIA MR. IBU AOMBA MSAADA WA FEDHA ZA MATIBABU

Muigizaji mkongwe kutoka nchini Nigeria, John Ikechukwu, maarufu Mr. Ibu ameweka wazi kuwa anapambana na ugonjwa unaotishia maisha yake huku akiwaomba watu kumsaidia pesa kwa ajili ya matibabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share video hiyo akizungumza akiwa hospitalini kwa kuomba msaada kwa mashabiki wake waweze kumchangia na kufichua kuwa kufuatia ugonjwa alionao huenda ukasababisha kukatwa miguu.

Mwaka 2022, aligunduliwa na ugonjwa wa kisukari na figo na alifanyiwa upasuaji katika kituo cha matibabu ya figo cha Zenith huko Abuja.


Mr. Ibu aliacha kushiriki katika kazi za sanaa mwaka 2019 kwa sababu ya ugonjwa huo. Katika moja ya mahojiano yake alieleza kuwa aliwahi kuwekewa sumu kwenye chakula na watu wa kijijini kwako kwa sababu ya wivu wa mafanikio yake.

Wapenzi wa filamu  walimtambua Mr. Ibu kupitia movie zake kama The Collaborator akiwa na Aki na Ukwa, Mr Ibu, My Chop Money na nyengine nyingi.

Post a Comment

0 Comments