Zaidi ya viongozi 200 wa soka duniani na Afrika kwa ujumla wamethibitisha kuhudhuria mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League utakaoikutanisha timu ya Simba dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Mchezo huo inatarajiwa kuchezwa Oktoba 20,2023 kwenye uwanja wa Mkapa, jijinj Dar es Salaam.
Viongozi watakaoshuhudia moja kwa moja mchezo huo ni Rais wa Shirikisho la Soka Duniania (FIFA) Gianni Infantino, Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura, kocha wa zamani wa timu ya Arsenal ya England, Arsene Wenger, Makamu mkuu wa Rais wa FIFA, Salman Bin Ibrahim Al Khalifa na Makamu wa Rais wa FIFA, Alejandro Dominguez.
Kwa upande wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) watakaokuja ni Rais wa CAF, Patrice Motsepe, Katibu Mkuu wa CAF, Veron Mosengo Omba, Makamu wa Rais wa CAF, Augustine Senghor, Ahmed Yahaya na Saidoo Mbombo.
0 Comments