Ticker

7/recent/ticker-posts

MWANAMKE AJIFUNGUA KUKU KIGOMA

Picha ya maktaba

Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke ambae jina lake halikutajwa ambae ni mkazi wa Uvinja mkoani Kigoma, amejifungua kuku.

Mwanamke huyo ambae inaelezwa kuwa hakuwahi kuwa na dalili za ujauzito amejifungua kuku katika kituo Cha Afya Uvinza.

 

Alifika hospitalini hapo ili kupewa huduma ya kujifungua baada ya kudai kuwa anasikia uchungu ambao ni kawaida kwa Wajawazito wakikaribia kujifungua.

 

Akiwa katika kupewa huduma ya uzazi ndipo alipojifungua kuku. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Chacha ndie amethibitisha tukio hili na kusema kuwa mama huyo alifika akiwa na mume wake.

 

"Mama huyu haoneshi dalili zozote kwamba alikuwa na ujauzito cha kushangaza zaidi kiumbe hicho hakihusiani na mfuko wa uzazi isipokuwa baada ya vipimo imeonekana mama huyo ana uvimbe kwenye kizazi taarifa zisizo rasmi zinasema aliingiziwa kuku huyo na Mganga wa kienyeji, tumewasiliana na vyombo vya usalama kufuatilia tukio hilo"

 

Ameeleza zaidi kwamba tukio hili linahusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa vipimo vinaonesha Mama huyo hakuwa na ujamzito na baada ya kutolewa kuku huyo ameendelea kutoa harufu mbaya katika sehemu ya uzazi, tayari ameagiza Mganga mfawidhi ampeleke hospitali ya Rufaa Maweni kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi . 

 

Post a Comment

0 Comments