Ticker

7/recent/ticker-posts

NDANI YA MIEZI MITATU TRA YAKUSANYA TRILIONI 6.58


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 6.58 ambayo ni sawa na asilimia 97.53 katika kipindi cha miezi mitatu cha robo ya kwanza ya mwaka mpya wa fedha wa 2023/24.

Lengo la makusanyo kwa kipindi hicho lilikuwa ni shilingi trilioni 6.75, makusanyo hayo ya robo ya kwanza yam waka mpya wa fedha ni sawa na ongezeko la asilimia 11.05 ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi trilioni 5.92 yaliyofikiwa katika kipindi kama hiki katika mwaka wa fedha wa 2022/23.

Kwa mujibu wa taarifa ya TRA iliyotolewa kwa umma leo Oktoba 3, 2023 na kusainiwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Bwa. Alfayo Kidata, katika kipindi cha mwezi Septemba 2023 walifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 2.63 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 108.41 ya lengo la kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 2.42, makusanyo haya ni ongezeko la asilimia 15.49 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi trilioni 2.27 kilichokusanywa katika mwezi kama huu katika mwaka wa fedha wa 2022/23. 

TRA imeanisha sababu nne zilizochangia kufikia malengo hayo kuwa ni pamoja na kutekeleza maelekezo na miongozo mbalimbali inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Aidha imewashukuru na kuwapongeza walipa kodi wote walioonesha uzalendo wa hali ya juu kwa nchi.

 

Post a Comment

0 Comments