Ticker

7/recent/ticker-posts

MUSEVENI AFURAHISHWA NA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA TANZANIA NA UGANDA

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amesema ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania umekuwa na mafanikio makubwa ya kihistoria na kiuchumi.

Akizungumza baada ya kupokea zawaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Uganda Museveni ameishukuru Tanzania na kusisitiza uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi pamoja na viongozi wengine kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.

Post a Comment

0 Comments