Ticker

7/recent/ticker-posts

SERIKALI KUPITIA UPYA ADHABU YA MWAKINYO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro  amesema kuna haja ya kufuatilia mwenendo wa mashtaka ili kubaini uhalali wa adhabu iliyotolewa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) dhidi ya bondia Hassan Mwakinyo. 

Dkt.Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) jijini, Dar es Salaam. 

“Wizara tutakaa na BMT na TPBRC, ili kuweza kupata taarifa rasmi ya nini kimetokea na misingi ya hiyo adhabu, baada ya kupata taarifa hiyo ndipo tutashauriana na wahusika wote namna adhabu hiyo ilivyotolewa, uhalali wake kama adhabu hiyo ni sahihi ataitumikia, iai kama kuna mushkeli kidogo tutakaa na kushauriana kuona tunafanyaje,” amesema Waziri huyo.

Oktoba 10, 2023 TPBRC ilitangaza kumfungia Mwakinyo ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya Sh milioni moja kwa kinachoelezwa Septemba 29 mwaka huu, bondia huyo aligomea kupanda ulingoni katika pambano lililofahamika ‘The Return of Champ’ huku pambano lake likiwa ndio kuu.

Post a Comment

0 Comments