Ticker

7/recent/ticker-posts

YANGA YAANZA LIGI KIKATILI, GAMOND AIBADILI KABISA SAFU YA USHAMBULIAJI


Kikosi cha Yanga kimeonesha mwelekeo mpya wa upachikaji magoli, ambao sasa haumtegemei mtu mmoja kama ilivyokuwa kwenye misimu miwili iliyopita, ambapo Fiston Mayele ndie alikuwa akitegemewa zaidi.

Ni wazi kocha raia wa Argentina Miguel Angel Gamond imeonesha mwelekeo  wake mpya ambao unaondoa kabisa utegemezi wa mchzaji mmoja katika kuleta matokeo.

Mchezo wa Ligi ya mabingwa na huu wa  Ligi Kuu ya NBC uliochezwa leo Agosti 23,2023 kwenye uwanja wa Chamazi, umeonesha mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji kama ilivyo pia safu ya ulinzi ambapo sasa hata beki anaowezo wa kupachika bao na hata mshambuliaji ana uwezo wa kushuka na kulinda ngome yao.

Mabadiliko hayo yaliyofanywa na Gamond yamewalazimisha KMC kuadhibiwa kikatili kwa kupigwa bao tano na hawakuweza kupachika hata bao moja.

Dickson Job ndie alikuwa wa kwanza kuifungia Yanga katika dakika ya 17, bao la pili lilipachikwa na Aziz Ki katika dakika ya 59.

Wachezaji wa Yanga waliendelea kuonesha uwezo wa kupachika mabao katika dakika ya 71 kupitia kwa Haliz Konkon, akifuaiwa na Mudathir Yahya aliyepeleka msiba kwa KMC katika dakika ya 76 na Pacome Zou zoua alihitimisha karamu ya magoli katika dakika ya 81.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuanza ligi kwa kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza katika michezo ya awali kupachika mabao mengi ndani ya mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya NBC ndani ya msimu wa 2023/24 bila kufungwa.

Mpaka sasa baadhi ya timu za Ligi Kuu  zimeshacheza mchezozaidi ya mmoja huku Yanga ikianza mchezo wake wa kwanza leo.

Post a Comment

0 Comments