Rasmi Nchi ya India imefanikiwa zoezi lao la kutuisha au kufikisha chombo chao kwenye upande wa south pole Mwezini ambapo inakuwa ni Nchi ya 3 kufanikisha kutuisha chombo Mwezini .
Safari ya India kuelekea Mwezini ilianza katikati mwa mwezi wa saba ambapo wametumia karibu siku 30 kuweza kufanikisha safari yao ambapo inakuwa ni hatua kubwa kwa Nchi ya India katika mbio za Kulitawala anga la mbali Kulikuwa na vyombo viwili ambapo vyote vilikuwa vipo katika harakati ya kutua katika upande wa south pole mwezini huku chombo cha Urusi Luna 25 kilishindwa kufanikiwa ambapo leo hii tumeshuhudia chombo cha Chandrayaan 3 kikifanikiwa kutua katika upande huo wa Mwezi
Sasa China Marekani na India ndio Nchi pekee ambazo zimefanikisha kutuisha vyombo Mwezini huku Marekani akienda mbali zaidi ya wote kwa kufanikisha kutuisha binadamu na China na India wao wakifanya mission za robot tu
China ipo mbioni kupeleka wanadamu katika miaka michache ijayo ambapo kama watafanikiwa basi itakuwa ni nchi ya pili bada ya Marekani
Mara baada ya kufika mwezini nchi ya India sasa watashusha kigari chao cha uchunguzi ambapo kitaweza kutembea katika maeneo ya huko South Pole mwezini pengine kitaweza kuona mabaki ya chombo chao cha Chandrayaan 2 kilipoangukia kwa maana hichi cha leo kimetua karibuni kabisa .
Ni jambo jema kwa India kufanikisha kitu kikubwa cha kisayansi .
Kama utakuwa na darubini kubwa na yenye nguvu basi huenda unaweza kuona chombo cha India kikiwa upande wa Mwezi unapotuangalia .
0 Comments