KUBWA KULIKO YA MWAKA.
Mwaka 1664 Meli Ilizama Katika Mlango Bahari wa Menai Huko Wales,Abiria Wote Walizama Kasoro Mmoja tuu Aliyeitwa Hugh Williams. Mwaka 1785 Meli Nyingine Ikazana Hapo, Aliyepona ni Mmoja,Hugh Williams.Mwaka 1820 Meli Nyingine Ilizama Tena, Aliyepona ni Hugh Williams.
Kuna historia hii ya ajali ya meli zilizowahi kuzama katika mlango wa bahari wa Menai karibu na pwani ya Wales, meli 3 zimepotea kwa miaka tofauti tofauti.
Na licha ya kupishana miaka hiyo lakini zote zilipotea tarehe hiyo hiyo moja, Desemba 5, na anaepona ni mmoja anaeitwa Hugh Williams
Desemba 5, 1664 meli ilizama katika mlango wa bahari wa Menai ikiwa na watu 81.
Kila mtu alizama na kufa majini lakini jina la manusura pekee lilikuwa ni Hugh Williams.Desemba 5, 1785 ikiwa ni miaka 121 baadae meli nyingine ilizama kwenye mlango wa bahari wa Menai ikiwa na watu 60 huku kila mtu ndani akifa isipokuwa mtu mmoja tuu aliyeitwa Hugh Williams.
Desemba 5, 1820 tena miaka 35 mbele meli nyingine ilizama kwenye mlango wa Menai ikiwa na watu 25, mtu mmoja tu ndiye aliyeokoka, na aliitwa Hugh Williams.
Historia imeandika kuwa baadaye pia meli nyingine mbili zilizama hapo hapo na mmoja wa watu waliopona jina lake lilikuwa ni hilo hilo Hugh Williams japo hizo hazikuzama tarehe hiyo ya December 5.
Matukio haya yote yamebaki kuandikwa katika vitabu pekee na kuhesabiwa kama ni mojawapo ya matukio ya kushangaza duniani, hakuna aliyewahi kuelezea lolote kuhusu jina hilo la Hugh Williams.
C&P
0 Comments