Ticker

7/recent/ticker-posts

YANGA VS KAIZER CHIEF KIUFUNDI ZAIDI

WananchiDay, Yanga 1-0 Kaizer

Na Sistiinho

Gamondi siku ya kwanza mbele ya Wananchi, Mbinu zake;

WAKIZUIA

Wasipokua na mpira huwa kwenye mfumo wa 4-1-4-1 na sio muumini wa kuzuia kwa shinikizo kubwa kuanzia mbele (Pressing)

Ni muumini wa timu yake kuanza kuzuia katikati, kwenye theluthi ya pili ya uzuiaji (Mid Block), Yanga waliwasubiri Kaizer wajenge shambulizi hadi katikati wao wakiwa wengi na hawajaachiana nafasi kubwa (Compactness)

Kwenye muundo wao uzuiaji wa 4-1-4-1, wachezaji walifanya majukumu yafuatayo;

-Mshambuliaji wa kati Musonda/Mzize huzuia njia kati ya mabeki wa kati wa Kaizer na viungo wao.

- Viungo wanne nyuma ya mshambuliaji, wa kati Nzegeli na Mudathir (2nd half Farid na Sureboy) huwazuia kwa ku-mark viungo wawili wa Kaizer wasiweze kuendeleza shambulizi, wa pembeni  Skudu na Nkane (Moloko na Ngushi) hu-track mikimbio ya full back wa Kaizer wakishambulia mapana ya uwanja kutotengeza 2v1 kwa full-back wa Yanga

- Kiungo wa Kati Mkude/Mauya huzuia kiungo mshambuliaji wa Kaizer anayeshambulia nafasi nyuma ya viungo washambuliaji na kutomruhusu kuwafikia mabeki wake

WAKISHAMBULIA

Wakiwa na mpira Yanga wakishambulia na mfumo wa 4-3-3 ambao ulinyumbulika kulingana na mpira unapokua

- wakijenga shambulizi kuanzia nyuma Metacha/Diara huwa Katikati ya mebeki kwenye muundo wa 3+4, mabeki wa pembeni huwa usawa wa viungo wa kati

- Wakifika katikati mfumo wao huwa 3-4-2-1, Mkude/Mauya Katikati ya CB, mbele yake mstari wa watu wanne, viungo wawili washambuliaji (Muda + Nzegeli/ Sureboy + Farid) na CB wawili Kibwana na Kibabage (Yao + Lomalisa) halafu mbele washambuliaji wawili wa pembeni Skudu + Nkane (Ngushi + Moloko) kati Musonda/Mzize

 Mapungufu ya kimbinu kwa Yanga ni;

- Wachezaji wa upande wa kulia 2nd half, Yao na Moloko wote hukumbatia chaki hakuna anayependa kuingia ndani kushambulia nafasi kati ya wachezaji wa pembeni na wa kati wa Kaizer, tatizo hili liliathiri flow ya timu

- Ufanisi na umakini wakutengeneza na kumalizia nafasi

 Performance za wageni

- Mkude 8/10

- Skudu 7/10

- Kibabage 7/10

- Nzegeli 8/10

- Yao 6/10

Wanahitaji mwendelezo bora

 Ile Kaizer haitwai taji lolote kwa Mamelod Sundowns

Post a Comment

0 Comments