Mwanamuziki wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Emmanuel Elibariki 'Ney wa Mitego', ameanza kukumbana na mkono wa sheria baada ya Leo Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) kutoa taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusu uamuzi wao wa kuzuia wimbo wake wa "Amkeni".
TCRA imeagiza wimbo huo kutopigwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya habari.
TCRA imeeleza kwamba ilipokea Malalamiko kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwa wimbo huo una maudhui yasiyofaa yanayoweza kusababisha uchochezi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake.
Wimbo huo wa Ney umebeba maudhui yenye taswira ya kuukosoa na kuusema vibaya uongozi na viongozi wa nchi.
0 Comments