Ticker

7/recent/ticker-posts

​ROMA MKATOLIKI AANDIKA 'BARUA' YA KUMKANA NEY WA MITEGO

Baada ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elbariki,' Ney wa Mitego' kudai kuwa baadhi ya mistari iliyomo kwenye  wimbo wake mpya wa "Amkeni" ambao unatajwa kubeba uchochezi alitumiwa na Mwanamuziki mwenzake  Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki, hatimae msanii huyo anaeishi Marekani kwa sasa amemkana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Roma amekanusha tuhuma hizo, ambapo ameandika

"YAH: SUHUSIKI KWENYE HILI

Kwenu Basata Tanzania, husika na kichwa cha Habari hapo juu, huyu kijana NAY ni muongo sana, mimi sijamtuma kitu chochote wala sijahusika kwenye wimbo wake huo, kwanza hata namba yake ya simu sina, ananisingizia na sijapenda, mimi ni kijana muadilifu sana na mnalijua hilo toka kuzaliwa kwangu, Basata Tanzania"

"Naipenda sana nchi yangu, zidumu fikra za Mwenyekiti na kazi iendelee 

#NB Akija huyo Jumatatu malizaneni naye peke yake, mimi nina familia na watoto wananitegemea kupitia huu mziki sitaki HEKAHEKA saizi!! 

Kwanza mimi urafiki na mtu FREEMASON wapi na wapi jamani, Basata Tanzania hata nyie hamuoni!!"- ameandika Roma.


Post a Comment

0 Comments