Ticker

7/recent/ticker-posts

MANDONGA SASA AMERUDI KWENYE KIWANGO CHAKE

Bondia wa Tanzania, Karim Mandonga maarufu kama Mtu Kazi sasa amerejea kwenye kiwango chake cha kudundwa katika kila pambano.

Mandonga ambae anatambulika zaidi kwa maneno mengi kabla na baada ya pambano hatimae  yamemkuta tena baada ya kupigwa kwa Technically knock out (TKO) katika  raundi ya tatu na bondia Moses Golola kutoka Uganda.

Hilo ni pambano la pili mfululizo kwa Mandonga kupoteza baada ya siku kadhaa zilizopita kuchezea kichapo kutoka kwa Daniel Wanyonyi wa Kenya katika pambano la marudiano jijini Nairobi.

(Picha zote kwa hisani ya Azam Media).


Post a Comment

0 Comments