Ticker

7/recent/ticker-posts

KINANA AWASHANGAA MADIWANI, WABUNGE AAMUA KUWATETEA

Hatua ya wabunge na madiwani nchini kujiita waheshimiwa imemsukuna Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana kuwashangaa na kudai kuwa hiyo ndio  inawaponza kwa wapiga kura wao

Kinana amesema wachaguliwa hao wanaponzwa na hatua yao ya  kujiita waheshimiwa na ndio maana wanaombwa sana fedha.

Ameyasema hayo kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika  jana mkoani Tabora.

Kinana alishangazwa na madiwani kujiita waheshimiwa wakati hata mishahara hawana.

“Madiwani wanalipwa posho tu, hawana mishahara, wanajiita waheshimiwa bila sababu na hapo ndipo  mtu akiwa na shida yake binafsi anaenda kwa diwani ampe hela, anauguliwa, diwani ndio atoe pesa ya matibabu, ana safari zake binafsi, diwani ndio atoe pesa, akisema hana, nongwa inaanzia hapo na kumwambia  watakukana kwenye uchaguzi 2025."

Aidha Kinana aliwatetea wabunge  wa Tanzania kuwa ndio wanaolipwa mshahara mdogo kuliko wabunge wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema nchi za DRC- Congo, Kenya, Uganda na  Rwanda  mishahara ya wabunge wake iko juu kuliko wabunge  wa Tanzania.

"Ikitokea  tukasema tuwaongeze mishahara, mtasikia kelele kutoka kwa watu, lakini ajabu Wabunge wakirudi jimboni kila mtu anapiga hodi akitaka apewe hela, wakati mwingine mtu anafunga safari kwenda anakokujua mwenyewe, lakini nauli hana na antaka mbunge ndio ampe, akimwambia sina basi nongwa inaanzia hapo na anaweza kumwambia 2025 tunakutoa.

Kinana alisema hiyo si sawa.

Post a Comment

0 Comments