Ticker

7/recent/ticker-posts

KOCHA YANGA APATA HOFU NA WASHAMBULIAJI ALIO NAO

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga muajentina Gamondi amesema kwa muda wa wiki mbili walizokaa kambini Avic Town amechunguza idara zote za kikosi chake na kugundua kuwa kwasaaa Yanga haina mshambuiiaji halisi anayeweza kuwa tegemeo.

 Kikosi kimeimarika idara zote sina hofu na timu kabisa.. Washambuliaji wa pembeni wapo,  watu wa kutengeneza nafasi wapo,  hofu yangu ni watu wa kuzitumia nafasi zinazotengenezwa. Ligi za ndani mara nyingi huwa za kawaida,ukikosa kuitumia nafasi unaweza kuipata tena na tena na hatimaye kwenye nafasi kadhaa ukafunga goli moja. Lakini mashindano ya kimataifa unakutana na kila timu nzuri zote,  ambazo sio rahisi kukupa nafasi za kufunga mara kwa mara,  hivyo unatakiwa kuwa na mchezaji ambaye akipata nafasi anafanya jambo.

Mara kadhaa nimepitia video za mechi za Yanga,  nimekuwa nikishangazwa na uwezo wa Fiston Mayele, ni aina ya wachezaji wanaotakiwa kwenye kikosi cha malengo,  ni bahati mbaya ameondoka. Nimeshaongea na uongozi wa Yanga wamenihakikishia kabla ya dirisha kufungwa watasajili mchezaji mwenye ubora kama Mayele au zaidi ya Mayele.

Post a Comment

0 Comments