Tofauti na ilivyoelezwa awali kuwa jezi nambari 20 iliyokuwa ikitumiwa na Jonas Mkude ndani ya kikosi cha Simba kuwa ingepumzishwa hadi hapo atakapopatikana mrithi wake ambae alipaswa kuwa chipukizi mzawa, hatimae jezi hiyo imekabidhiwa kwa Che Malone Fondoh.
Che ni mlinzi mpya wa Simba na Jana ameonekana kutinga jezi yenye namba 20 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Turan PFK nchini Uturuki
Awali Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally alitangaza kustastaafisha matumizi ya jezi namba 20 katika klabu hiyo kwa kile kilichoelezwa kuheshimu mchango Mkude baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa takribani miaka 13.
Hata hivyo leo Julai 28,2023, Ahmed Ally alisema walitimiza ahadi ya kumpa jezi chipukizi wao kama walivyoahidi, lakini chipukizi huyo aliiona Che ndio anaestahili zaidi kuvaa jezi namba 20 ndani ya uwanja.
0 Comments