Ticker

7/recent/ticker-posts

MZEE BUTIKU AJITOSA SAKATA LA MKATABA WA BANDARI

Baadhi ya nukuu za Mzee Butiku kwenye kipindi cha Dakika 45 hapo jana;

1. Ninavyojua mimi mkataba ulisainiwa Oktoba 2022 na huenda ulikua siri ndio maana mwanzoni watanzania hawakujua yaliyokuwemo.

2. Inasemekana mkataba ume-leak, labda ni kweli. Maana kama viongozi wangekua na nia ya kuuleta kwa wananchi kwanini waulete mwaka mmoja baada ya kusaini?

3. Kwa maoni yangu Watanzania wengi hawataki bandari ipewe DP World.

4. Kama tatizo la bandari yetu ni kukosa ufanisi na usimamizi mbovu je kubinafsisha ndio suluhisho?

5. Watanzania wanasema bandari ni mali yetu na urithi wetu, na hawapendi kuona urithi wao ukichezewa.

6. Hoja za mgawanyiko zinazoibuka kuhusu uwekezaji wa bandari hazipaswi kuzimwa kwa vitisho.

7. Serikali ikumbuke imepewa mamlaka na wananchi na haiwezi kujiamulia tu mambo wananchi wasiyotaka. Kabla serikali haijaamua lazima ijiulize hiki ndicho wanachi wanachokitaka?

8. Bandari ni mpaka wetu ni usalama wetu. Wakumbuke Mwalimu alisema Bandari na viwanja vya ndege ni malango ya nchi. Kumleta mtu Bandarini ni sawa na kumwingiza mgeni chumbani kwako.

9. Viongozi wasidhani wana akili kuliko wananchi hivyo wakapuuza maoni yao. Hawaongozi kuku wala mbuzi, wanaongoza watu wenye utashi na upeo mkubwa kuliko wao.

10. Tukipiga kura hili la bandari mimi nitasema HAPANA, HAPANA, HAPANA. Tukubali kujisahihisha hata kama ni kwa gharama.!

Credits: #Jmshinga na @mbowejames

Post a Comment

0 Comments