Ticker

7/recent/ticker-posts

WAZIRI AFUTA AGIZO LA KUWATOZA MILIONI MOJA WANAUME WANAOSUKA NYWELE ZANZIBAR

Siku moja baada ya Serikali ya Mapinduzi ZanIbar, kupitia kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni, Dkt Omar Adam kutangaza utaratibu wa wanaume wanaotaka kusuka nywele zao, hatimae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita, ameomba radhi na kutengua agizo hilo. 

Jana  Dkt. Omar Adam alitangaza kuwa  mwanaume yeyote anayetaka kusuka visiwani humo itambidi alipie kiasi cha shilingi milioni moja ili kupata kibali cha kufanya hivyo.

Akitengua agizo hilo leo, Waziri Tabia amesema Katibu Mtendaji huyo aliteleza na kwamba Zanzibar inasimamia sheria inayotaka kulinda mila na utamaduni wa Mzanzibar na ipo kanuni inayoeleza katika mipaka ya Zanzibar wanaume wa Kizanzibar kusuka ni kinyume na mila, utamaduni na desturi na yeyote atakayekiuka hayo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ama kifungo cha miezi 6.

Waziri huyo amesema kwamba Wizara yake itaendelea kuheshimu tamaduni za watu wengine ikiwemo pia kuzingatia haki za binadamu na kwamba sheria za Zanzibar ziko palepale kwamba mila, silka na tamaduni kuendelea kulindwa.

Post a Comment

0 Comments