Mchezaji wa zamani wa Simba, Jonas Gerald Mkude, ameukataa hadharani mpango wa klabu ya Simba wa kutaka kumuaga kwa heshima siku ya Simba Day.
Mkude ameachwa na Simba aliyoitumikia kwa zaidi ya misimu 10 kwa kile kilichodaiwa ni kumpa nafasi akatafute changamoto mpya.
Katika moja ya kurasa zake za mitandao ya Kijamii, Mkude ameandika "Kwa heshima niliyopewa na wananchi sihitaji hata kuagwa kwa heshima siku ya Simba Day."
0 Comments