Ticker

7/recent/ticker-posts

USHABIKI NA SIFA ZASABABISHA MABASI KUFUTIWA RATIBA YA KUANZA SAFARI USIKU

Mamlaka ya Udhibiti Usarifi Ardhini -LATRA, imesitisha ratiba ya kuanza safari za mikoani saa tisa usiku kwa mabasi tisa. 

Uamuzi huo umetangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa  LATRA,  CPA Habibu Suluo Juni 19,2023.

Kwa mujibu wa taarifa ya LATRA, mabasi hayo yamechezea mfumo wa king'amuzi (Vehicle Tracking System - VTS) na kusababisha mwendo kasi,hali inayohatarisha usalama wa abiria wanapokuwa safarini.

Uamuzi huo ni kwa mujibu wa  Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini chini ya kifungu cha 5 (1) (b) na 6 (b) Sura ya 413, ambayo imeipa Mamlaka jukumu la kutoa, kuhuisha na kufuta vibali na leseni za usafirishaji.

Pia kifungu cha 16 (b) kimeipa Mamlaka wajibu wa kukuza usalama wa sekta zinazodhibitiwa na usalama wa watumiaji wa huduma hiyo.

Mabasi yaliyofutiwa ratiba hiyo ya usiku ni ya kampuni  ya Ally's Star mabasi sita na  Kampuni ya Katarama Express mabasi matatu.


Kampuni ya Isamilo yenyewe  imepewa onyo kali kwa kuwa matukio yao hayajakithiri.

LATRA imewasihi wananchi kuacha tabia ya kushabikia vitendo vinavyo hatarisha usalama na uhai wa abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Aidha amewakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi kuzingatia sheria za utoaji wa huduma katika usafiri wa umma.

Post a Comment

0 Comments