Ticker

7/recent/ticker-posts

GWAJIMA 'APIGANIA' BARABARA ZA BRT JIMBONI KWAKE

Mbunge wa Kawe, Akofu Josephat Gwajima leo ameendeleza dhamira yake ya kuwaletea maendeleo wapiga kura wake kwa kuitaka serikali kumpa uhakika wa ni lini Jimbo lake litapata Barabara za mabasi ya mwendo wa haraka (BRT).

Katika swali lake la nyongeza Gwajima alimuuliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya kuwa ni lini serikali itajenga kipande cha Barabara hiyo kinachounganisha Mwenge na Basihaya.

"Ni lini serikali itajenga Barabara ya Mwendo Kasi ya BRT Form ambavyo kipande kikubwa kinaanzia Mwenge, Makongo Sekondari, Lugalo Jeshini, Mbezi Beach, Tegeta kwa Ndevu, Nyaishozi mpaka Basihaya ambayo pia itaonoa mafuriko yanayoikumba Basihaya kwa kujenga mitaro."


Akijibu swali hilo Mhandisi Kasekenya alisema barabara hiyo imo kwenye mpango wa BRT.

"Barabara aliyoitaja iko Kwenye BRT Form ambayo itaanzia Maktaba, itakuja Mwenge mpaka daraja la Kijazi, hii itakuwa ni Lot ya kwanza.

"Lot ya pili itaanzia Mwenge, Tegeta kuja Dawasa na kutakuwa na wakandarasi wawili.

" Lot ya tatu ni mkandarasi wa Majengo na tarehe 30 Ijumaa ya Mwezi huu pale Dawasa tunakwenda kusaini mikataba ya kuanza ujenzi wa barabara ya BRT Form."

Hatua hiyo ya Gwajima kuulizia barabara hiyo ni Mwendelezo wake wa kuwasemea wapiga kura wake ndani ya Bunge hasa kwenye masuala hyanayogusa maendeleo yao moja kwa moja.

Post a Comment

0 Comments