Ticker

7/recent/ticker-posts

VIJANA WOTE WA KIDATO CHA SITA WAITWA JKT

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawaita vijana wote walihitimu kidato cha sita mwaka 2023,  kuanza kuripoti Juni Mosi hadi 11 mwaka huu katika makambi ya Jeshi hilo kwa ajili ya mafunzo ya kwa mujibu wa sheria._ 

Hatua ya kuita wanafunzi wote kutoka shule za Bara waliohitimu kidato cha sita mwaka huu 2023, imekuja baada ya kuboresha miundombinu mbalimbali._ 

Tangazo hilo limetolewa leo tarehe 25 Mei, 2023 na Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Rajabu Mabele._ 

Amesema wahitimu Wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wametakiwa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina  miundombinu ya kuhudumia watu wa Jamii hiyo._ 

Mbali na hayo,jeshi hilo,limewataka vijana hao kuja na bukta ya rangi ya Dark blue yenye kiuno iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini  isiyo na zipu na vingine ambavyo vimeanishwa._ 

Brigedia Jenerali Mabena,ametaja makambi ambayo wanafunzi hao  wanatakiwa kuripoti ni pamoja na JKT Rwamkoma (Mara),JKT Msange -(Tabora),JKT Ruvu (Pwani),JKT Mpwapwa, Makutupora JKT (Dodoma),JKT Mafinga (Iringa) na JKT Mlale  (Ruvuma)._ 

Kambi nyingine ambazo wanafunzi hao wanatakiwa kuripoti ni JKT Mgambo,JKT Maramba (Tanga),JKT Makuyuni,Orjolo JKT(Arusha),JKT Bulombora,JKT Kanembe,na JKT Mtabila (Kigoma),JKT Itaka (Songwe),JKT Luwa,Milundikwa -(Rukwa),JKT Nachingwea (Lindi) JKT Kibit_ 

Vingine ni track suit ya rangi ya kijana au bluu, nyaraka zote zinazohitajika katika usajili wa kujiunga na elimu ya juu, zikiwemo vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kuhitimu kidato cha nne._ 

Amesema utaratibu kupata walizopangiwa umerahisishwa ambapo kijana ataandika majina yake matatu aliyotumia kwenye mtihani na kupata jina la kambi alilopangiwa na eneo lilopo._

Post a Comment

0 Comments