Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa wawekezaji wanaokusudia kuanzisha biashara zao Zanzibar washirikiane na jamii kusaidia masuala mbalimbali kama vile elimu, maji na afya.
Dk. Mwinyi amesisitiza kwamba wawekezaji wanapaswa kuona umuhimu wa kusaidia jamii inayowazunguka pale wanapowekeza, na kuhakikisha kwamba wanachangia kwa hali na mali ili kuboresha uhusiano wao na jamii hiyo.
Ameyasema hayo leo baada ya swala ya Ijumaa katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid El-Marhoum Abdel Moeim Shahein uliopo Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika hotuba yake Rais Dk. mwinyi alibainisha kuwa nia na madhumuni ya msikiti huo ni kutoa fursa ya kufanya ibada na kuwafundisha vijana katika madrasa iliyopo msikitini hapo.
0 Comments